# Kwa sababu hii Neno "hii" linarejea kwa ahadi ya Bwana kulazimisha manabii wa uongo nje ya Israeli. # wamewaongoza watu wangu Neno "wao" linarejea kwa manabii wa uongo katika nchi ya Israeli. # wanajenga ukuta ambao wataupaka chokaa Hapa "ukuta" unasimama kwa ajili ya amani na ulinzi ambao manabii wa uongo wamewaambia watu kwamba Yahwe aliahidi kuwapatia. # kupaka chokaa ... chokaa "chokaa" ni kimiminika cheupe kilichochanganywa kwa kufanya sehemu ya juu ya kitu (kama vile kuta au wigo) # mvua ya kufurika ... mvua ya mawe ... upepo wa dhoruba Haya yote ni sehemu ya dhoruba mbaya sana. Mungu anatumia dhoruba kurejea majeshi yatakayoishambulia Yerusalemu. # mvua ya mawe vigololi vya barafu ambavyo wakati mwingine vinaanguka kutoka angani kipindi cha dhoruba ya mvua. # wengine hawakukwambia Ezekieli anauliza hili swali kushinikiza jibu.