# Maelezo ya jumla Malaika amemaliza kuongea, na Danieli anaendelea kusema kile alichokiona baadaye katika maono yake tangu katika 10:4 # kulikuwa na malaika wengine wawili wamesimama "kulikuwa na malaika wengine wawili wamesimama" # Mmoja wao alimwambia mtu aliyevaa nguo za kitani, Hii inamrejelea mtu aliyekuwa akiongea na Danieli, siyo mmoja wale watu waliokuwa wamesimama pembeni mwa mtu. # ukingo wa mto, Maana zinazoweza kukubalika 1) malaika alikuwa juu ya mto au 2) malaika alikuwa mbali katika ukingo sambamba na mto. # Je itachukua muda gani mpaka mwisho wa matukio haya ya kushangaza? "Matukio haya ya kushangaza yatadumu kwa muda gani?" Hii inarejelea mwanzo hadi mwisho wa matukio. # matukio haya ya kushangaza Katika muda ule ambao malaika alikuwa akiongea na Danieli, hakuna hata tukio hata moja lilikuwa limetokea. Hii kwa uhalisia inarejelea matukio katika 12:1, na huenda yalijumuisha matukio yaliyo katika maono kutoka sura ya 11.