# kasirike na kughadhabika Maneno haya kimsingi yanamaanisha kitu kile kile na kutia mkazo juu ukali wa hasira yake. # wale wote katika Babeli "watu wote katika Babeli" # Hivyo, amri ilitoka Amri inaongelewa kama ni kitu chenye uhai na chenye uwezo wa kwenda nje. "Mfalme aliipitisha amri" # wale wote waliojulikana kwa hekima yao ni lazima wauawe Hii yaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "Wanajeshi walitakiwa kuwaua watu wote waliojulikana kwa hekima zao" # ili kwamba wauawe Hii inaweza kuelezwa kwa muundo tendaji. "kwa lengo la kuwaua"