# Maelezo yanayounganisha Festo akaendelea kuongea na Mfalme Agripa # Nimemleta kwenu, hasa kwako, Mfamle Agripa " Nimemleta Paulo kwenu nyote lakini hasa kwako Mfalme Agripa" # Ili nipate cha kuandika zaidi "ili nipate cha ziada cha kuandika" au "ili nijue niandike nini" # haina maana kumpeleka mfungwa na bila kuonyesha mashitaka yanayomkabili "itakuwa na maana nikimpeleka mfungwa na kuonyesha mashtaka yanayomkabili" # Mashitaka dhidi yake inamaanisha kuwa 1) mashitaka yaliyoletwa juu yake na viongozi wa Kiyahudi au 2) mashitaka chini ya sheria za Roma yanayoelezea kesi ya Paulo.