# Sentensi unganishi Paul alimaliza kumjibu Gavana Feliki kuhusu mashtaka yaliyowasilishwa dhidi yake. # wanaume hawahawa Hii ina maana ya wajumbe wa baraza ambao walikuwepo Kaisaria katika kesi ya Paulo. # lazima waseme kosa waliloliona kwangu "waseme iwapo kuna kitu kibaya nilikifanya na kukithibitisha" # Ni kuhusu ufufuo wa wafu neno "ufufuo" linaweza kutumika kama "Kurudishwa katika maisha na Mungu." Na, neno "wafu" linaweza kuwa "wale waliokufa." "wakati Mungu akiwarudisha katika uhai wale wote waliokuwa wamekufa" # Ninahukumiwa leo na wewe hii inaweza semwa kama "mnanihukumu mimi leo hii"