# Mji wote ulikuwa na taharuki Neno "wote" hapa ni lugha ya kuumba picha kubwa kwa msisitizo. neno "mji" inawakilisha watu katika mji huo. "Watu wengi katika mji wakawa na hasira juu ya Paulo." # "Walimvamia Paulo" Paulo alivamiwa # milango mara ikafungwa Walifunga milango ili kwamba kusije kufanyika maandamano ndani ya hekalu. # habari zilimfikia mkuu wa kikosi cha ulinzi afisa wa kikosi cha ulinzi au kiongozi wa askari wapatao 600 # Yerusalemu yote ilikuwa katika ghasia Neno "Yerusalemu" hapa inawakilisha watu wa Yerusalemu. neno "wote" ni msisitizo kuonyesha umati mkubwa waliokuwa wamekasirika. "wengi wa watu huko Yerusalemu walikuwa katika ghasia."