# nikiwa ninamtii Roho Mtakatifu kuelekea Yerusalemu, nisiyajue mambo ambayo yatanitokea mimi huko, Hapa anaongelea juu ya Roho Mtakatifu akimshawishi Paulo kwenda Yerusalemu kama vile Roho Mtakatifu alikuwa amemfunga mfano wa mtumwa. # Roho Mtakatifu hunishuhudia mimi Roho Mtakatifu amewasilisha maonyo haya kwangu # minyororo na mateso ndivyo vinavyoningojea Mimi nahusika kufungwa jela kwa minyororo na kuteswa katika kifungo. # ili niweze kumaliza mwendo wangu na huduma niliyopokea kutoka kwa Bwana Yesu Paulo anatumia mfano waq mashindano. Ili kukamilisha kazi ambayo Mungu aliiweka kwa ajili ya yake kuifanya # kuishuhudia injili ya neema ya Mungu "kuwaambia watu habari njema kuhusu neema ya Mungu. Hii ndiyo huduma ambayo Paulo alikuwa ameipokea kutoka kwa Yesu.