# Taarifa unganishi Paulo na wenzake wakaendelea na safari yao # Taarifa ya jumla Fungu hili linazungumzia juu ya Luka na wale waliokuwa wakisafiri naye bila Paulo kuwemo kwenye kundi. # Sisi wenyewe tulikwenda Neno 'wenyewe' linaongeza mkazo na hutenganisha Luka na wasafiri wenzake Paulo, ambaye hakusafiri kwa mashua # tulisafiri kwenda Aso Aso ni mji uliokuwa chini ya mji wa Behram ya sasa katika Uturuki pwani ya bahari ya Aegean. # yeye mwenyewe alitamani "yeye mwenyewe" ni kiwakilishi cha jina la Paulo aliyekuwa anatamani # kwenda kwa njia ya bara Kusafiri kwa nchi kavu # kwenda Mitylene Mitylene ni mji katika siku ya leo Mitilini, Uturuki katika pwani ya bahari ya Aegeana.