# Sentensi unganishi Huu ni mwisho wa sehemu ya habari inayowahusu Wayahudi wapunga mapepo. # Wakakusanya vitabu vyao 'Walikusanya vitabu vyao'. Neno "vitabu" linaelezea aina ya magombo yaliyokuwa yakitumika kuendeshea manuizio ya uchawi kutokana na mwelekezo wa maneno yaliyoandikwa humo. # mbele ya macho ya kila mtu mbele ya kila mtu # thamani yake "thamani ya vitabu" au "thamani ya yale magombo" # Elfu hamsini 50,000.00 # vipande vya fedha "Kipande cha fedha" ilikuwa takriban mshahara wa siku kwa mfanyakazi wa kawaida # Hivyo Neno la Bwana likaenea kwa upana sana katika njia yenye nguvu "Kwasababu ya matendo makuu haya, watu wengi zaidi waliusikia ujumbe kuhusu Bwana Yesu."