# Taarifa ya jumla Hii ni sehemu nyingine ya hadithi ya safari ya Paulo. Kwa sasa yuko Corintho. Akwila na Priskila wanatambulishwa kwenye hadithi katika mstari 2 na 3 inatoa habari ya nyuma kuhusu wao. # baada ya mambo hayo, "baada ya matukio hayo kufanyika huko Athene" # Huko akampata Inaweza kuwa na maana kwamba: 1) "Paulo alitokea kumpata kwa bahati" au 2) "Paulo alimpata baada ya kuwatafuta kwa nia.' # Mtu mmoja aliyeitwa Akwira Hapa anamtaja mtu yule aliyemwona huko naye ni Akwira. # mzaliwa wa Ponto Ponto ilikuwa mkoa katika pwani ya kusini ya Bahari ya Nyeusi. # alikuwa amehamia karibuni "Hii huenda ni muda fulani kwa miaka ya nyuma" # Italia Jina hili ni la nchi. Roma ni mji mkuu wa Italia. # Klaudia alikuwa ameagiza Klaudia alikuwa ndiye Kaisari wa Kiroma kwa sasa. # Alikuwa akifanya biashara waliyoifanya Alikuwa akifanya aina ya kazi waliyoifaya na wao.