# mitume, Barnaba na Paulo Inawezekana Luka anatumia "mtume" katika hali ya ujumla ya "yule ambaye ametumwa." # walichana nguo zao Hili ni tendo la ishara kuonesha kuwa walihuzunishwa na kukasirishwa kwamba kundi lilitaka kuwatolea wao sadaka. # Watu, kwa nini mnafanya hivi vitu? Barnaba na Paulo wanawakaripia watu kwa kujaribu kuwatolea sadaka. "watu, hampaswi kutuabudu!" # Sisi pia ni binadamu wenye hisia kama nyie Kwa kauli hii, Baranaba na Paulo wanasema kuwa wao sio miungu. "Sisi ni binadamu tu kama nyie.. Sisi sio miungu!" # wenye hisia sawa na nyie "kama nyie kwa kila hali" # mgeukieni Mungu aliye hai kutoka kwa vitu hivi visivyo na maana "acheni kuabudu miungu ambayo haiwezi kuwasaidia, na badala yake anzeni kumuabudu Mungu aliye hai" # Mungu aliye hai "Mungu ambaye kweli yupo" au "Mungu anayeishi" # Siku za nyuma "katika nyakati za zamani" au "Hadi sasa" # kutembea katika "kuishi kulingana na"