# Maelezo ya jumla Viwakilishi vya majina hapa vinamuwakilisha Paulo na kundi lote la watu waliokuwemo kwenye Sinagogi. # Ndugu, watoto wa ukoo wa Abrahamu, na wale ambao kati yenu mnamwabudu Mungu Paulo analielezea kundi la Wayahudi na wale wa mataifa walioungia katika dini ya kiyahudi ili kubaki na hali yao waliyoichagua ya kumwabudu Mungu wa kweli. # ujumbe huu wa ukombozi umetumwa Kwa maneno mwngine; "Mungu ameshatuma ujumbe wake wa wokovu" # Ukombozi huu Neno hili linamaanisha kwamba; "Mungu atawaokoa watu" # hawakumtambua "Hawakuweza kabisa kumtambua huyu mtu Yesu alikuwa ni mmoja ambaye Mungu alimtuma kuwakomboa." # Ujumbe wa manabii. Unawakilisha; "Maandiko ya manabii" au "Ujumbe wa manabii." # ambao unasomwa "Ambao mtu anausoma" # walitimiliza ujumbe wa manabii "Hakika walitenda kama vile Manabii walivyosema."