# Sentensi unganishi Paulo anamalizia majadiliano na Elima. # mkono wa Bwana upo juu yako Neno "mkono" unawakilisha nguvu za Mungu na neno "juu yako" linamaanisha adhabu . "Mungu atakuadhibu" # utakuwa kipofu. Hii inaweza kutafsiriwa kuwa; "Mungu atakufanya kipofu" # Hautaliona Jua Elima atakuwa kipofu kabisa kwamba hataweza kuliona jua. # kwa muda "Kwa kipindi fulani" au "Mpaka muda wa Mungu aliouamru" # mara moja ukungu na giza vilianguka juu ya Elimas "Macho ya Elima yakapata ukungu na giza" au "Elima uoni ulikuwa hafifu na kisha hakuweza kuona kabisa" # alianza kuzunguka pale "Elima alianza kutangatanga" # Liwali Huyu alikuwa ni mtumishi wa serikali katika jimbo la Rumi. # Aliamini "Alimwamini Yesu" # alishangazwa kwa mafundisho kuhusu Bwana. "Mafundisho kuhusu Bwana Yesu yalimshangaza mno"