# nikasikia sauti Sauti ilinena lakini bila yeyote kujidhihirisha. "Sauti" yawezekana ni Mungu, ingawa inawezekana kuwa ilikuwa sauti ya Malaika. # Siyo hivyo "Siwezi kufanya hivyo" linganisha na sura 10:13. # mdomoni mwangu hakujawahi kuingia kitu chochote kisicho kitakatifu Wanyama waliokuwa kwenye kitambaa walikuwa ni wanyama ambao sheria ya Wayahudi katika Agano la Kale iliwazuia wasiweze kuwala. # Kichafu Katika Agano la Kale Sheria ya Wayahudi, mtu alionekana mchafu katika njia mbalimbali, kama vile kula wanyama waliokuwa hawaruhusiwi kuliwa. # kile Mungu alichokitangaza kuwa ni safi, usikiite najisi Sentensi hii inaelezea juu ya wanyama waliokuwa kwenye kitambaa kikubwa cha pembe nne. # Hii ilitokea mara tatu Si kila tukio lilirudiwa kuonekana mara tatu, Hata hivyo neno; "Kile Mungu alichokitakasa usikiite najisi" Ni neno lilijirudia mara tatu kwa Petro. Linganisha na sura 10:13.