# Sentensi unganishi Petro anawajibu Wayahudi kwa kuwaambia juu ya maono na kile kilichotokea katika nyumba ya Kornerio. # Petro alianza kueleza Petro hakujaribu kusema maneno ya kuwapinga Wayahudi waumini, bali alijibu kwa maelezo ya kirafiki na hekima. # Kwa undani "Hakika ya kile kilichotokea" # Kama kitambaa kikubwa Chombo kilichoshikilia wanyama kilionekana kitambaa kikubwa. # Chenye pembe nne "Kikubwa chenye pembe nne" # wanyama wenye miguu minne waishio katika nchi, "Wanyama wa miguu" Mwitikio wa Petro ulilenga sheria ya Musa iliyokuwa inazuia kula baadhi ya wanyama. # Wanyama wa mwitu Pengine ni wanyama wasioweza kufugwa. # wanyama watambaao Hawa ni wale waendao kwa kutambaa.