# Sentensi unganishi Huu ni mwisho wa sehemu ya simlizi kuhusu Kornerio. # wamataifa wanaongea kwa lugha zingine na kumwabudu Mungu Zilijulikana kuwa ni lugha zilizokuwa zinatamkwa na waliojazwa na Roho Mtakatifu, kilichofanya Wayahudi kukubali kwamba wamataifa nao walikuwa wakimtukuza Mungu. # Kuna mtu yeyote anaweza kuzuia maji ili watu wasibatizwe, Watu hawa wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi? Petro alilitumia swali hili kuwashawishi Wayahudi wakristo kwamba Wamataifa walioamini wanaweza kubatizwa. # Ndipo akawaamuru wabatizwe Inamaanisha kwamba Wayahudi wakristo ndio waliowabatiza Wamataifa siku hiyo. # wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo "Kwa Jina la Yesu Kristo" Linaelezea kuwa sababu ya kubatizwa kwao ni kwa kumwamini Yesu Kristo.