# Sentensi unganishi Petro anaendelea na Kornerio pamoja na wageni wake. # ambaye ni Bwana wa wote "Wote" maana yake watu wote" # Yudea yote "Katika maeneo mbalimbali ya Yudea" # baada ya ubatizo ambao Yohana alitangaza "Baada ya Yohana kuhubiri kwa watu kurubu na kubatizwa" # Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na kwa nguvu Roho Mtakatifu na nguvu za Mungu zimenenwa kana kwamba ni vitu vinaweza kumiminwa juu ya mtu. # wote walioteswa na ibilsi "Watu wengi waliokuwa wanapitia mateso ya shetani" # Mungu alikuwa pamoja naye. Inamaanisha; "Mungu alikuwa akimtia nguvu kuzitenda kazi zote"