# sauti ikasema kwake Mtu anayeongea hajulikani. Pengine "sauti" alikuwa Mungu mwenyewe, ingawa inawezekana alikuwa Malaika kutoka kwa Mungu. # Siyo hivyo Petro anaapa "Sitafanya hivyo" # sijawahi kula kitu chochote najisi na kichafu Imetafsiriwa kuwa wanyama wanawakilisha wasio safi kama ilivyoelezwa na sheria ya Musa na walikuwa hawaliwi na waumini walioishi kabla ya kifo cha Kristo. # Alichokitakasa Mungu Kama Mungu ndiye msemaji, anajipambanua mwenyewe kwa nafsi ya tatu; "Kile ambacho Mungu alikitakasa" # Hii ilitokea mara tatu Si kwamba kila kitu alichokiona Petro kilitokea mara tatu. Hii inaweza kuwa na maana; "Kile ambacho Mungu alikitakasa" neno hili ndilo lilijirudia mara tatu mfurulizo.