# Sentensi unganishi Huu ni mwanzo wa sehemu juu ya habari inayohusu Kornelio. # Maelezo ya jumla Mistari hii inatupa mrejesho wa taarifa kuhusu yeye. # Kulikuwa na mtu fulani Hii ilikuwa ni njia ya kutambulisha mtu mwingine katika habari. # jina lake aliitwa Cornelio, alikuwa mkuu wa kikosi cha Kiitalia "jina lake aliitwa Kornelio. alikuwa ni mtu mwenye cheo wa maaskari 100 kutoka Italia katika sehemu ya jeshi la Rumi" # Alikuwa mcha Mungu na alimwabudu Mungu "Aliamini katika Mungu na alitaka kumtii Mungu na kumwabudu Mungu katika maisha yake" # na nyumba yake yote "na watu wote wengine wa nyumbani kwake ambao pengine walikuwa wa mataifa walimcha Mungu" # aliomba kwa Mungu siku zote. Alikuwa akimwomba Mungu wakati wote.