# Mitume kumi na wawili Hapa wanazungumziwa mitume kumi na moja pamoja na Mathias aliyekuwa amechaguliwa. # kusanyiko lote la wanafunzi "Wanafunzi wote" au "Waumini wote" # Siyo sahihi kwetu kuliacha neno la Mungu Ni neno lenye msisitizo wa muhimu wa kutokuacha huduma ya kufundisha neno la Mungu # Kuhudumia meza Hili ni neno kwa ajili ya kuhudumia chakula kwa watu. # Wanaume wema, waliojawa na Roho na hekima Uwezekano wa maana waweza kuwa 1) Wanaume wana sifa tatu- wema, kujazwa na Roho, na kujazwa na hekima au 2) wanaume wana tabia njema kwa sifa mbili- kujazwa na Roho, na kujawa na hekima. # kuwakabidhi huduma hii. Kuwa na wajibu kwa huduma hiyo muhimu. # huduma ya neno Ni huduma ya kufundisha na kuhubiri habari njema.