# Sentensi unganishi Viongozi wa dini walianza kuwatesa waumini # Lakini Neno "lakini" linaanzisha habari kinzani. Unaweza kutafasiri hii kwa namna ambavyo lugha yako hutambulisha habari kinzani. # kuhani mkuu aliinuka, Neno "kuinuka" linamaanisha Kuhani mkuu aliamua kuchukua hatua, si kwamba aliinuka tu kutoka kwenye kiti chake alichokikalia. # na walijawa na wivu Inamaanisha walijawa na wivu sana # wakanyosha mikono yao kuwakamata mitume Waliwakamata mitume kwa nguvu, kwa kuwa walikuwa wameagiza walinzi wao wapate kuwakamata mitume.