# Sentensi unganishi Maelezo ya namna wakristo walivyokuwa wakishirikiana mahitaji kwa baadhi ya wakristo kuuza mali zao. Luka anatuambia habari za waumini wawili Anania na Safira walivyohusika katika ushirika huo. # Sasa "Lakini sasa." Hii inaonyesha sehemu kumalizika na kuanza kwa maelezo ama habari mpya. # Mke wake pia alilijua "Mke wake pia alijua kuwa Mmewe alikuwa ametunza nyumbani sehemu ya fedha kwa mauzo ya shamba lao". # kuiweka kwenye miguu ya mitume. Inamaanisha kwamba waliwasilisha hiyo fedha kwa mitume.