# Sasa Hapa Petro anageuza usikivu wa mkutano kutoka kwa kiwete na anaendelea kuwaambia moja kwa moja. # kwamba mlitenda katika ujinga Maana inayowezekana 1) Hao watu hawakujua kuwa Yesu alikuwa Masihi au 2) Watu hawakujua maana ya kile walichokuwa wakifanya. # Mungu aliwaambia mapema kwa vinywa vya manabii wote Manabii waliponena, ilikuwa kama Mungu mwenyewe aliyenena kwasababu aliwaambia nini cha kusema. # kwa mdomo wa manabii wote Inamaanisha yale yote yaliyonenwa "kupitia manabii" na kuyaandika.