# Matendo 02: Maelezo ya Jumla ### Muundo na mpangilio Tafsiri zingine zimesongeza kila mstari wa ushairi mbali kulia kuliko maandiko mengine ili isomeke kwa urahisi. ULB hufanya hivi kutumia ushairi ulionukuliwa kutoka Agano La Kale katika 2:17-21,25-28 na 34-35. Tafsiri zingine zimenukuu kutoka Agano la Kale katika mkono wa kulia wa ukurasa mbali na maandishi mengine. ULB hufanya hivi kutumia nukuu ya 2:31 Matukio yanayofafanuliwa katika sura hii huitwa "Pentekoste." Watu wengi huamini kwamba kanisa lilianza wakati Roho Mtakatifu alikuja kuishi ndani ya waumini katika sura hii. ### HANA MAALUM KATIKA SURA HII #### NDIMI Neno "ndimi" lina maana mbili katika sura hii. Luka anaelezea kilichoshuka kutoka mbinguni (Matendo 2:3) kama kilichofanana na ndimi za moto. Hii ni tofauti na "ulimi wa mwale," ambao ni moto unaofanana na ulimi. Luka pia anatumia neno "ndimi" kuelezea lugha walizozungumza watu baadaya kujazwa na Roho Mtakatifu (Matendo 2:4-6). #### SIKU ZA MWISHO Hakuna ajuaye wakati "Siku za mwisho" (Matendo 2:17) zilipoanza. Tafsiri yako lazima isielezee zaidi ya ULB inavyoeleza. (Tazama: rc://en/tw/dict/bible/kt/lastday) #### Batiza Neno "batiza" katika sura hii linaashiria ubatizo wa Wakristo (Matendo 2:38-41). Ingawa tukio lililotajwa katika Matendo 2:1-11 ni ubatizo wa Roho Mtakatiu ambao Yesu aliahidi katika Matendo (1:5, neno "batiza" hapa halikuashiria hilo tukio (tazama: rc://en/tw/dict/bible/kt/baptize). #### Unabii wa Yoeli Utabiri mwingi wa Yoeli ulitimilika katika siku ya Pentekoste (Matendo 2:17-18), lakini vitu vingine alivyosema Yoeli havikutendeka (Matendo 2:19-20). (Tazama: rc://en/tw/dict/bible/kt/prophet) #### Maajabu na ishara Haya maneno yanaashiria mambo ambayo Mungu pekee yake angeyatenda kuonyesha kwamba Yesu ndiye yule wanafunzi wake walinena juu yake. ## Links: * __[Acts 02:01 Notes](./01.md)__ __[<<](../01/intro.md) | [>>](../03/intro.md)__