# Sentensi unganishi Tukio hili lilitukia wakati Petro na waumini wengine walikuwa pamoja katika chumba cha juu. # Katika siku zile Maneno haya yanaashiria mwanzo mpya wa historia. Yanaelezea kipindi baada ya Yesu kupaa na wakati wanafunzi wakiwa katika chumba cha juu wamekutanika kuomba. # katikati ya ndugu Neno "ndugu" Linaelezea ndugu waumini likiunganisha wanawake kwa wanaume. # ilikuwa lazima kwamba maandiko yatimizwe Yale mambo tunayoyasoma katika maandiko lazima yatimizwe # kwa kinywa cha Daudi Neno "kinywa" Linaelezea yale maneno aliyoyasema Daudi.