# Sentensi unganishi. Luka anaelezea ni kwasababu gani anamwandikia Theofilo # Kitabu cha zamani nilikiandika Kitabu cha zamani ni Injili ya Luka. # Theofilo Luka aliandika kitabu hiki kwa mtu anayeitwa Theofilo. Baadhi ya watafsiri hufuata mfumo wa tamaduni zao za kuelezea barua na huandika "Mpendwa Theofilo" mwanzoni mwa sentensi. Theofilo humaanisha "rafiki wa Mungu. # Mpaka siku alipopokelewa juu Hii inarejesha kwenye kupaa kwa Yesu mbinguni # Amri kupitia kwa Roho Mtakatifu Roho Mtakatifu alimwongoza Yesu kuwaelekeza mitume wake juu ya vitu fulani. # Baada ya kuteswa kwake Hii inahusu mateso ya Yesu na kifo chake msalabani. # Alijidhihirisha Yeye mwenyewe akiwa hai Yesu alionekana kwa mitume wake na kwa wanafunzi wengi wengine.