# ndipo mwenye kuasi atakapofunuliwa Hii inaweza kusemwa katika muundo tendaji. AT: Halafu Mungu atamruhusu mwenye kuasi ili kujionyesha mwenyewe. # kwa pumzi ya kinywa chake Hapa neno "pumzi" linamaanisha nguvu ya Mungu. AT: "kwa nguvu ya neno lake lilotamkwa" # Ufunuo wa kuja kwake utamfanya kuwa sio chochote Wakati Yesu atakaporudi duniani na kujionyesha, atamshinda yule mwenye kuasi. # kwa nguvu zote, ishara, na maajabu ya uongo "kwa nguvu zote, ishara, na maajabu ya uongo" # na uongo wote wenye udharimu Mtu huyu ataumia kila aina ya ubaya kuwadanganyawatu ili wamwamini yeye badala ya Mungu. # Mambo haya yatakuwepo kwa wale wanaopotea Huyu mtu atapewa nguvu na shetani na atadanganya kila mtu ambaye hakuamini katika Yesu. # wanaopotea Hapa "potea" lina wazo la milele au uangamivu wa milele