# Ndipo Israeli wote Hii inawahusu askari wa Israeli na siyo Waisraeli wote. # tutaleta kamba juu ya mji huo na kuukokotea mtoni, hata kusionekane hata jiwe moja dogo lililosalia Hii inamaanisha kwamba askari wangeuangusha mji chini na kukokota vipande vyake katika mto # hata kusionekane hata jiwe moja dogo lililosalia. Hii ni kutia chumvi kwa kueleza ni jinsi gani watakavyouangamiza mji. Hii siyo katika hali halisia. # Hushai Mwarki Huyu ni rafiki wa mfalme Daudi. Arki ni jina la kundi la watu katika Israeli # Ahithofeli hili ni jina la mshauri wa Daudi # Kukataliwa kwa shauri jema la Ahithofeli Neno "kukataliwa" linaweza kuelezwa na kitenzi "kataa" # kulete angamizo juu ya Absalomu "Kuleta" kitu fulani juu ya mtu inamaanisha kusababisha jambo kufanyika kwake.