# hata hivyo Ijapokuwa Bwana ni mvumilivu na anataka watu watubu, hakika atarudi na kuleta hukumu. # siku ya Bwana itakuja kama mwizi Petro anazungumza juu ya siku ambayo Mungu atamhukumu kila mmoja kama mwizi anayekuja pasipo kutegemewa na kuwashtusha watu. # Mbingu itapita kwa kupaza kelele "Mbingu zitapita" # Vitu vitateketezwa kwa moto Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu atateketeza kwa moto" # Vitu Maana zinazowekana ni 1) vitu vya mbinguni kama vile jua, mwezi, na nyota au 2) vinavyofanya mbingu na nch, kama vile mchanga, hewa, moto na maji. # nchi na matendo yatafunuliwa Mungu ataiona dunia yote na matendo yote ya kila mmoja, na atahukumu kila kitu. Hii inaweza kusemwa katika kauli tendaji. "Mungu ataiweka wazi nchi na kila kitu watu walichofanya."