# kwa kuupima uhalisi wa upendo wenu kwa kuulinganisha na shauku ya watu wengine Paulo anawatia moyo Wakorintho kutoa kwa ukarimu wao kwa kuulinganisha na ukarimu wa makanisa ya Makedonia. # neema ya Bwana wetu Katika mukutadha huu neno "neema" linasisitiza ukarimu wa Yesu Kristo amewabariki Wakorintho. # Hata kama alikuwa tajiri, kwa ajili yenu alikuwa maskini Paulo anamzungumzia Yesu kabkla hajafanyika mwanadamu alivyokuwa tajiri, na kwa kufanyika mwanadamu kama kuwa maskini. # kupitia umaskini wake mweze kuwa tajiri. Paulo anazungumzia Wakorintho kuwa matajiri kiroho kama matokeo ya Yesu kuwa mwanadamu.