# 2 Wakorintho 07 Maelezo ya Jumla ### Muundo na upangiliaji Katika mistari ya 2-4, Paulo anamaliza kujitetea kwake. Halafu anaandika juu ya kurudi kwa Tito na faraja iliyoletwa. ### Dhana maalum katika sura hii #### Usafi na uchafu Wakristo ni "wasafi" kwa maana kwamba Mungu amewatakasa kutoka kwa dhambi. Hawakuhitaji ya kuwa na wasiwasi ya kuwa safi kulingana na sheria ya Musa. Kuishi kwa ukafiri huweza kumfanya Mkristo kutokuwa msafi. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/clean]] and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/lawofmoses) #### Huzuni na masikitiko Maneno "huzuni" na "masikitiko" katika sura hii yanaonyesha kwamba Wakorintho walikuwa wamesononeka kiasi cha kutubu. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/repent) ### Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii #### Sisi Labda Paulo anatumia neno "sisi" kuwakilisha Timotheo na yeye mwenyewe. Au labda anawajumuisha watu wengine pia. #### Hali ya awali Sura hii inazungumzia kwa kina hali nyingine ya awali. Tunaweza kufikiria mambo fulani ya hali hii kutokana na taarifa katika sura hii. Lakini ni bora kutoingiza aina hii ya habari kamili katika tafsiri. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-explicit) ## Links: * __[2 Corinthians 07:01 Notes](./01.md)__ __[<<](../06/intro.md) | [>>](../08/intro.md)__