# Habari za Jumla Paulo anaorodhesha mitazamo mingi jinsi watu wanavyofikiri juu yake na huduma yake. # Tunatuhumiwa kuwa wadanganyifu Sentensi hii inaweza kuelezwa kwa jinsi hii: "watu hutushtaki kwa kuwa wadanganyifu" # kana kwamba hatujulikani na bado tunajulikana vizuri. Sentensi hii inaweza kuelezwa kwa jinsi hii: "ikiwa kama watu hawakututambua sisi na bado watu wanatutambua vizuri" # Tazama! Neno "Tazama" linatukumbusha kusikiliza kwa makini habari za kushangaza zinazofuata. # Tunafanya kazi kama tunaoadhibiwa kwa ajili ya matendo yetu lakini sio kama vile waliohukumiwa hata kufa. Sentensi hii inaweza kuelezwa hivi": "tunatemda kazi kama vile watu wanatuadhibu kwa matendo yetulakini siyo kama vile wametuhukumu kufa"