# Sentensi unganishi: Paulo anaendelea kumuasa Timotheo awajali wanaume, wanamke, wajane na wanawake wazee ndani ya kanisa. # Taarifa ya jumla: Paulo alikua anatoa maagizo haya kwa mtu mmoja, Timotheo. # Usimkemee mwanaume mzee. "Usiongee kwa ukali kwa mzee wa kiume" # Ila msihi kama baba "Ila mtie moyo kama uongeavyo na baba yako," kwa adabu. # Msihi kijana wa kiume kama ndugu "Mtie moyo vijana wa kiume kama ndugu zako" au "wafundishe vijana wakiume kama ambavyo ungefundisha ndugu zako," kwa amani. # Wanawake vijana kama dada "wasihi wanawake vijana kama ambavyo unge wasihi dada zako" au "wafundishe wanawake vijana kama ambavyo ungewafundisha dada zako," # Kwa usafi wote "kwa mawazo safi na matendo" au "katika hali ya utakatifu"