# Watoto wapendwa. Watoto wanaopendwa/waumini wanaopatana naye. # Msiruhusu mtu yeyote kuwapotosha. "Msikubali mtu yeyote awafanye wajinga" au "msikubali mtu yeyote awadanganye." # Atendaye haki ni mwenye haki, kama Kristo alivyo mwenye haki. "Anayetenda kilicho sahihi anampendeza Mungu kama Kristo anavyompendeza Mungu." # Hutenda dhambi. "Huendelea kutenda dhambi" # Ni ya Ibilisi. "Humilikiwa na shetani au ni kama shetani" # Kutoka mwanzo. Hii inalenga hasa nyakati za uumbaji kabla ya binadamu hawajaanguka dhambini. "Tangu nyakati za mwanzo za uumbaji." # Mwana wa Mungu alidhihirishwa. Hii inaweza kutafsiriwa kwa fungu la maneno yanayoonesha kitendo: "Mungu alimudhihirisha Mwanawe." # Mwana wa Mungu. Hili ni jina mhimu kwa Yesu ambalo hufafanua uhusiano kwa Mungu.