# Sentensi Unganishi Yohana anaendelea kuandika juu ya ushirika na anaonyesha kwamba inawezekana kwa sababu Yesu yuko kati ya waaminio na Baba. # Maelezo ya Jumla Hapa maneno "tunaye' na "zetu" humaanisha Yohana na waaminio wote. Neno "Yeye" na "zake" yaweza kumaanisha Mungu Baba au Yesu. # Watoto Yohana alikuwa mzee na kiongozi wao. Alitumia maelezo haya kuonyesha pendo lake kwao. : "Watoto wangu wapendwa katika Kristo" au "Ninyi mliowapendwa kwangu kama watoto wangu mwanyewe" # ninawaandikia mambo haya "Ninaandika barua hii" # Lakini kama mmoja wenu akitenda dhambi "Lakini mmoja wenu anapotenda dhambi." Hili ni jambo ambalo inawezekana likatokea" # tunaye wakili aliye pamoja na Baba, Neno "wakili" hapa humaanisha Yesu. : "mtu anayezungumza kwa Mungu Baba na kumsihi yeye apate kutusamehe sisi" # eye ni upatanisho kwa dhambi zetu, na siyo kwa dhambi zetu "Aliyatoa dhabifu maisha yake mwenyewe kwa ajili yetu, na kwa sababu ya hilo Mungu husamehe dhambi zetu" # Kwa hili twajua kwamba , kama tukizishika amri zake. "Kama tunafanya anayotuambia kufanya, kisha tutakua na uhakika kwamba tunao uhusiano na yeye" # tunamjua yeye "tunao uhusiano na yeye"