# Sentensi unganishi Paulo anawakumbusha waumini wa Korintho kukusanya pesa kwa ajili ya waumini wenye mahitaji walioko Yerusalemu. Pia anawajulisha kuwa Timotheo atapitia kwao kabla ya kwenda kwa Paulo. # ya waumini Paulo alikuwa anakusanya pesa kutoka kwenye makanisa yake kwa ajili ya wakristo masikini wa kiyahudi huko Yerusalemu na Yuda. # kama nilivyo elekeza "kama nilivyowapa maelekezo mahususi" # aweke kitu fulani kando na kukihifadhi, Maana zinazowezekana ni: 1) " kitu hicho tunza nyumbani" au 2) "kilete kitunzwe kanisa" # ili kwamba kusiwe na makusanyo wakati nitakapokuja " kwa hiyo nitakapokuja hakutakuwa na haja ya kukusanya pesa zingine zaidi"