# Ni nani afanyaye kazi kama askari kwa gharama zake mwenyewe? " Wote tunajua kuwa askari hatumii vifaa vyake mwenyewe." au " Wote tunajua kuwa kila askari hupokea vifaa kutoka serikalini" # Ni nani apandaye mzabibu asile matunda yake? " Wote tunajua kuwa yule anayepanda shamba la zabibu atakula matunda yake." au " Wote tunajua kuwa hakuna anayetarajia mtu aliyepanda shamba la zabibu asile matunda yake." # Au na nani achungaye kundi asiyekunywa maziwa yake? " Wote tunafahamu kuwa wale wachungao kundi hupata kinywaji chao kutoka kundini." # Je ninasema haya kwa mamlaka ya kibinadamu? "Mnafikiri kuwa ninasema mambo haya kwa matakwa ya mamlaka ya kibinadamu." # Sheria nayo pia haisemi haya? "Mnatenda haya kana kwamba hamjui hivi ndivyo imeandikwa katika sheria."