# Sentensi Unganisha Paulo anaelezea anavyotumia uhuru wake katika Kristo # mimi si huru? Paulo anatumia swali kuwakumbusha Wakorintho juu ya haki alizo nazo. " mimi ni mtu niliye huru." # Mimi si mtume? Paulo anatumia swali hili kuwakumbusha Wakoritho juu ya vile alivyo na haki aliyo nayo. "Mimi ni mtume." # Mimi sikumwona Yesu Bwana wetu? Paulo anatumia swali hili kuwakumbusha Wakoritho juu ya vile alivyo. "Nimemuona Yesu Bwana wetu." # Ninyi si matunda ya Kazi yangu katika Bwana? Paulo anatumia swali hili kuwakumbusha Wakoritho juu ya uhusiano wao kwakwe. "Imani yenu katika Kristo ni matokeo ya kazi yangu katika Bwana." # ninyi ni uthibitisho wa utume wangu katika Bwana. " ninyi ni kielelzo ambao naweza kutumia kuthibitisha kuwa Bwana amenichagua kuwa mtume "