# Maelezo ya Jumla: Sura hii inaelezea vita ya mwisho kwa mji wa Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa. # mateka wenu watakapogawanywa katikati yenu Inamaanisha "Adui zenu watachukua mali yenu yote na kuigawana mbele yenu" # nitayakusanya mataifa yote kinyume cha Yerusalemu kwa vita "Nitayafanya mataifa kuishambulia Yerusalemu" # kumbukumbu ya watu haitaondolewa mjini "Adui zenu wataacha masalia kukaa katika mji"