# Maelezo ya Jumla: Mistari hii inaendelea na sehemu inayozungumzia shambulio lijalo dhidi ya Yerusalemu na jinsi Mungu atakavyouokoa mji. # siku hiyo Siku majeshi yatakapoishambulia Yerusalemu. # Hili ni tamko la Yahwe Kifungu hiki mara kwa mara kinafasiriwa kama "asema Yahwe" Kifungu hiki kimetumika mara nyingi katika kitabu cha Zakaria. # Nitaiangalia kwa upendeleo "Nitailinda" # nyumba ya Yuda "watu wa Yuda" # wasema mioyoni mwao Inamaanisha kwamba watafikiri na kujisemea wenyewe. # kwa sababu wa Yahwe wa majeshi "kwa sababu wanamwabudu Yahwe wa majeshi"