# Taji itawekwa katika hekalu la Yahwe "Nitaweka taji yangu katika hekalu langu" # Taji Neno "taji" inamtaja mfalme kama ambavyo mfalme angevaa taji. # iliwekwa katika hekalu la Yahwe Hii inahusu mfalme pia akiwa kuhani, kama kuhani anatumika hekaluni. # Heldai, Tobiya, na Yedaya Haya ni majina ya wanaume # kama kumbukumbu ya ukarimu wa mwana wa Zefania Baadhi ya matoleo ya kisasa yanafasiri kifungu hiki "kama kumbukumbu kwa Heni, mwana wa Zefania" au "kama kumbukumbu kwa mwenye neema, mwana wa Zefania." Pia, baadhi ya matoleo ya kisasa yanafasiri neno "Heni" kumaanisha jina "Yosia." # walioko mbali Hii inawahusu Waisraeli waliokuwa wamesalia Babeli. # hivyo utajua Neno "wewe" inamaanisha watu wa Israeli. # sikilizeni kweli "sikilizeni kwa uaminifu"