# Taarifa ya Kuunganisha: Malaika alinayeongea na Zakaria anaendelea kuelezea ono # Neno la Yahwe lilikuja "Yahwe alisema neno lake" # Mikono ya Zerubabeli... mikono yake itaimaliza Zerubabeli anasimamia ujenzi wa hekalu. Kujenga kunatajwa kama "mikono yake" japokuwa yawezekana mikono yake isiweke mawe. # kuweka msingi Msingi ni chanzo cha jengo na sehemu ya kwanza ya mradi wa ujenzi. # Ni nani aliyezarau... mambo madogo? Swali hili haliitaji jibu ila linawaambia wasizarau "siku ya mambo madogo." # siku ya mambo madogo Kifungu hiki ni jina kwa ajili ya wakati ambapo kila siku kazi rahisi zilifanywa. Muda wote wa ujenzi wa jengo unatajwa kama siku moja japokuwa ilichukua miaka kadhaa kukamilika. # Jiwe la kupimia Jiwe linalounganishwa na kamba. Linatumika kuamua kama kuta za jengo zimenyooka au hapana. # taa saba ni macho ya Yahwe Hizi taa saba ni alama za macho ya Yahwe. # macho ya Yahwe Neno "macho" linamtaja Mungu akiona kwa sababu macho hutumika kwa kuona.