# Kimbieni! kimbieni! Maneno haya yamerudiwa na yanaonesha umuhimu kwa ujumbe unaofata. Umetumika mara mbili kwa sababu ujumbe ni mhimu sana. # nchi ya kaskazini Inamaanisha Babeli # nimewatawanya kama pepo nne za anga Hii inamaanisha watu wa Israeli wako mbali mmoja kwa mwingine. Pepo nne zinamaanisha sehemu mbalimbali za dunia. # binti Babeli Hii inamaanisha mji mkuu wa Babeli.