# malaika mwingine akaenda kukutana naye Huyu ni malaika mwingine ambaye hajawai kutokea hapo mwanzo, na hivyo anatambulishwa kama mshiriki mwingine. # Malaika wa pili akamwambia, "Nenda uongee na mtu yule Malaika mwingine alimwambia malaika aliyekuwa ameongea na Zakaria, "Nenda haraka uongee na mtu mwenye kipimo" # Yerusalemu inakaa katika nchi wazi Kifungu hiki kinamaanisha kwamba Yerusalemu haitazungukwa na kuta. # kuwa kwake ukuta wa moto kumzunguka Yahwe anasema atailinda Yerusalemu na kulinganisha ulinzi wake na ukuta wa moto. # Hili ni tamko la Yahwe Kifungu hiki wakati mwingine kinatafasiriwa kama asema Yahwe.