# Nimeirudia Yerusalemu kwa rehema nyingi Kurudi Yerusalemu inamaanisha kuchukua tena jukumu la kuwaudumia watu wa Israeli kama mfalme kurudi kuwaongoza watu kutoka katika shida. # Nyumba yangu itajengwa ndani yake "Hii inamaanisha kujengwa tena kwa hekalu katika Yerusalem" # hili ni tamko la Yahwe wa majeshi Kifungu hiki mara kwa mara kinafasiriwa kama "asema Yahwe." Na kifungu hiki kimetumika mara kwa mara katika kitabu hiki. # Kipimo kitanyoshwa juu ya Yerusalemu "Yerusalemu itakaguliwa kabla ya kujengwa" # Miji yangu kwa mara nyingine itajawa na uzuri Yahwe anamaanisha mambo mema atakayoyafanya kwa ajili ya watu wake Israeli kama ambavyo kimiminika kinavyoweza kujaa katika miji na kufurika. # Yahwe ataifariji tena Sayuni "Yahwe atawatia moyo watu wa Israeli"