# Katika mwezi wa nane Huu ni mwezi wa nane katika kalenda ya Kiyahudi. Katika kalenda ya sasa ni mwishoni mwa Octoba na mwanzoni mwa Novemba. # mwaka wa pili wa kumiliki kwake Dario "mwaka wa pili tangu Dario alipokuwa mfalme" # Neno la Yahwe lilikuja "Yahwe alinena neno lake" # Berekia...Ido Haya ni majina ya wanaume. # Yahwe alikuwa na hasira sana juu ya baba zenu "Kuwakasirikia sana babu zenu" # Nirudieni Neno "rudi" inamaanisha mabadiliko. Yahwe anawaambia watu wa Israeli kubadilika kutoka kutokumtii na kumtii. # asema Yahwe wa majeshi Kifungu hiki mara kwa mara kitafasiriwa kama "asema Yahwe" katika UDB. Na kirai hiki kimetumika sana katika kitatu cha Zakaria. # Nitawarudia ninyi Kwa kusema atawarudia watu wa Israeli, Yahwe anasema watakuwa na mambo mema yakitokea kwa sababu atakuwa akiwasaidia.