# Sentensi unganishi: Paulo anaendelea kumpa Tito maelekezo juu ya namna ya kufundisha wazee na watu chini ya uangalizi wake huko Krete. # Uwakumbushe "Kuwaambia watu wetu tena kile ambacho tayari wanakijua" au "Kuendelea kuwakumbusha" # nyenyekea kwa viongozi na mamlaka, kuwatii "fanyeni kama watawala wa kisiasa na wenye mamlaka ya kiserikali wasemavyo kwa kuwatii" # watawala na wenye mamlaka Maneno haya yana maana zinazofanana na yametumika pamoja kumuhusisha kila mmoja ambaye anashikilia mamlaka katika serikari. # muwe tayari kwa kila kazi njema "muwe rayari kufanya mema wakati wote palipo na fursa" # ubaya "ongea mabaya juu ya" # waache watu wengine waenende katika njia zao Paulo anawasihi waumini kufanya mambo kama vile watu wengine wanavyopendelea kufanya, ilimradi tu matakwa yao na matendo yao yasiwe ya dhambi. "