# Sentensi kiunganishi Paulo anamtia moyo Tito kuutarajia ujio wa Yesu na kukumbuka mamlaka yake kupitia kwa Yesu. # neema ya Mungu imeonekana.....Inatufundisha Paulo anaiongelea neema ya Mungu kama ni Mtu anayeenda kwa watu wengine na kuwafundisha jinsi ya kuishi maisha matakatifu. # inatufundisha kukataa mambo yasiyo ya kimungu na tamaa za kidunia Inatufundisha tusimwasi Mungu # tamaa za kidunia "Hizi ni tamaa kali kwa ajili ya vitu vya dunia hii" au "tamaa kwa ajili anasa" # katika wakati huu "wakati bado tunaishi katika dunia hii" au " "muda huu" # tunatarajia kupokea "Tunasubiri kupokea" # tumaini letu lenye baraka, Paulo anamaanisha kwamba Mungu atakuja kwetu ambaye ndani yake tumeweka tumaini letu . # mwonekano wa utukufu wa Mungu wetu mkuu na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Paulo anaongelea juu ya utukufu wa Mungu kumaanisha kwamba Mungu mwenyewe atajidhihirisha.