# Sentensi unganishi Baada ya kuwa amekwisha kumwambia Tito kuwaweka kazini wazee katika kila mji katika kisiwa cha Krete, Paulo anatoa matakwa yanayohitajika kwa wazee. # Mzee lazima asiwe na lawama Kutokulaumiwa ni ilie hali ya kujulikana kuwa mtu huyo hatendi mambo mabaya. "Mzee lazima asiwe na sifa mbaya." # Mme wa mke mmoja "kuwa mme mwaminifu" Maana zinazokubalika 1) Mme ambaye hatafuti mahusiano na wanawake wengine au 2) asiye na mke wa pila au hawala au suria. # Watoto waaminifu Imaana zinazokubalika ni 1)watoto wanaomwaminiYesu au 2)watoto ambao ni waaminifu # wasio na nidhamu "waasi" au "ambao hawafuati maagizo" # msimamizi wa nyumba ya Mungu Paulo anaongelea juu ya wazee kana kwamba walikuwa vichwa vya familia, wakuu wa nyumba ya Mungu" # Asiye...zoelea pombe "asiwe mtu mwenye kutumia kileo" au "asiwe mnywaji" au "asiwe mlevi sana wa pombe" # Asiwe mgomvi "Asiwe mtu wa fujo"au "asiwe anapenda kupigana na kugombana"