# Maelezo ya Jumla Mwana mke anaendelea kuzungumza na mpenzi wake. # Nieka kama muhuri kwenye moyo wako, kama muhuri kwenye mkono wako Maana zinazo wezekana ni 1) Kwasababu mihuri ilikuwa muhimu, watu waliweka shingoni mwao au mikononi mwao. Mwanamke anataka kuwa na mwanamme wake kama muhuri. Au 2) Muhuri waonyesha nani anamiliki kitu chenye muhuri wake. Mwanamke anataka awe kama muhuri moyoni mwa mpenzi wake na mkononi ili kuonyesha mawazo yake, hisia, na matendo ni yake. # kwa kuwa mapenzi yana nguvu kama mauti Mauti ina nguvu sana kwasababu inawashinda ata watu wenye nguvu duniani. # hayana kurudi kama kwenda kuzimu Kuzimu hakuruhusu watu kurudia uhai baada ya kuwa wamekufa. Mapenzi yana msimamo kama kuzimu kwasababu hayabadiliki. # miale yake yalipuka ... kuliko moto wowote Mapenzi yana nguvu kama moto. # yalipuka "kuchomeka ghafla"